Kampeni uchaguzi mdogo Dimani zaanza


Salha Mohamed

Ramadhani Kailima
KAMPENI za uchaguzi mdogo katika Jimbo la Dimani kwa ngazi za ubunge na udiwani zinaanza rasmi leo.

Jimbo hilo lenye kata 20 linatarajia kufanya uchaguzi wake Januari 21, huku kata mbili za Mkoma na Mwamtani zikitolewa kwenye uchaguzi huo.

Akizungumza jana Dar es Salaam Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uhaguzi (NEC), Ramadhani Kailima, alisema kampeni hizo za kuchagua mbunge na madiwani zitakamilika Januari 21.

Alisema licha ya kuanza kwa kampeni leo orodha ya majina ya wagombea itawekwa wazi leo asubuhi.

“Kampeni za uchaguzi zitaanza kesho (leo) uteuzi wa wagombea mwisho ni leo (jana)  saa 10 jioni na orodha itatolewa kesho (leo)  asubuhi,” alisema Kailima.

Katika uchaguzi huo, kata za halmashauri za Tanzania Bara ni 20 zitashiriki, huku NEC ikibainisha kuwa kanuni ya 18(2) ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge ya Mwaka 2015 inaalika asasi na taasisi za ndani zitakazokuwa watazamaji wa uchaguzi huo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo