Bosi wa Jamii Forums apewa dhamana


Grace Gurisha

Maxence Melo
HATIMAYE muasisi wa mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo, ameachwa huru kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, baada ya  kukaa mahabusu kwa siku sita akishikiliwa na Polisi kwa mahojiano.

Melo aliachwa jana na Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa, baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya wadhamini wawili wa kuaminika ambao walisaini bondi ya Sh milioni tano kila mmoja, huku pia akitakiwa asitoke nje ya Dar es Salaam bila kibali cha Mahakama.

Baada ya mshitakiwa huyo kupata dhamana, ndugu, jamaa na marafiki walishindwa kujizuia wakaangua vilio vya furaha huku wakipongezena kwa kufanikisha dhamana ya ndugu yao.

Wakati Melo akitoka eneo hilo alionekana dhahiri kupepesuka, hali ambayo ilisababisha watu waliomzunguka wakiwamo baadhi ya wanasheria wake kumshikilia huku wengine wakimpa pole.

Melo akiwa mbele ya Hakimu Mwambapa, alidaiwa kuwa katika tarehe zisizofahamika kati Mei 10 na Desemba 13 alizuia upelelezi wa Jeshi hilo akikataa kukubaliana na amri za kutoa taarifa alizonazo kwenye mtandao wake.

Alidai kuwa akiwa ofisini kwake Mikocheni, akifahamu kuwa Polisi inachunguza makosa ya mitandaoni kupitia tovuti yake kinyume na sheria ya makosa mitandaoni, alikataa kutoa taarifa hizo za elektroniki.

Mbali na mashitaka hayo, pia anadaiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Thomas Simba, kwa mujibu wa Wakili wa Serikali Mwandamizi Mohamed Salum kuwa tarehe zisizofahamika kati ya Aprili mosi, na Desemba 13,Mikocheni, akiwa Mkurugenzi wa Jamii Media Ltd  ambaye ni mwendeshaji mtandao wa kijamii wa Jamii Forums alizuia upelelezi.

Katika kesi ya tatu, Melo alipandishwa kizimbani kujibu tuhuma mbele ya Hakimu Victoria Nongwa ambapo akituhumiwa mara mbili; kwanza kuzuia upelelezi na pili kuendesha mtandao bila kuusajili.

Salum alidai kuwa katika tarehe zisizofahamika, kati ya Desemba 9, 2011 na Desemba 13 mwaka huu akiwa Mikocheni aliendesha mtandao wa ‘jamiiforums.com’ bila kusajiliwa katika mtandao wa Tanzania (do-tz). Melo alikana mashitaka.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo