Mbowe asuka upya uongozi wa Chadema Kyela


Moses Ng’wat, Kyela

Freeman Mbowe
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amevunja uongozi wa chama hicho wilaya ya Kyela na kuteua safu mpya ili kunusuru chama hicho kupasuka kutokana na makundi yaliyotokana na uchaguzi mkuu uliopita.

Katika safu hiyo mpya itakayongozwa na mwanasiasa mkongwe, Lumuli Kasyupa, ambaye amewahi kuwa mbunge wa Kimbo la Kyela na Naibu Waziri wa Kilimo katika Serikali ya Awamu ya Kwanza ya hayati Mwalimu Julius Nyerere, kabla ya kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chadema.

Uamuzi huo wa Mbowe ulifanyika juzi kwenye ziara yake na mikutano ya ndani inayoendelea mkoani Mbeya kwa lengo la kukijenga chama hicho na kushughulika na mambo mbalimbali.

Mbali na Kasyupa ambaye alikuwa kada wa CCM na mbunge wa jimbo la Kyela kwa miaka 15, wengine waliochaguliwa ni Makamu Mwenyekiti, Philimon Mahenge, Katibu ni Mponjoli Mwaikimba, wakati katibu wa uenezi ni Donald Mwaisango maarufu kama Alfa na Omega na mweka hazina, Timoth Luvanda.

Wenyeviti wa mabaraza walioteuliwa ni mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (Bawacha), Tamali Mwambalaswa, Bavicha ni Yesaya Mwakalobo na Mwenyekiti wa Baraza la wazee Anton Mapunda.

Hata hivyo, Mbowe alionekana kukasirishwa na migogoro iliyokithiri ndani ya chama hicho na kusababisha kishindwe kufikia malengo yake ya kushika dola, huku  akitumia nafasi hiyo kuwaonya madiwani kwa uzembe.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo