Nyota wa Tanzania wanaocheza soka nje


Charity James

WACHEZAJI wa Tanzania wameamka sasa, wamekuwa wakitoka kwa wingi nchini kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kutafuta timu zenye malisho mazuri zaidi ya timu za hapa nyumbani.

Idadi hiyo ya wachezaji kuondoka nchini kwenda nje imekuwa kubwa tofauti na miaka mingine ambayo kulikuwa hakuna mchezaji anayecheza ligi katika nchi jirani.

Moja ya kitu ambacho tumekikosa kwa wakati huu ni kupata kundi kubwa la makocha ambao watakwenda kufundisha soka nje ya nchi, lakini kwa mwenendo uliopo sasa, Tanzania itakuwa na kundi la makocha ambao watakuwa wakifundisha soka nje ya nchi.

Nahodha wa kikosi cha Taifa Stars na mshambuliaji wa klabu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta ni baadhi ya wachezaji wa Tanzania ambao hivi sasa wanaipeperusha vyema bendera ya nchi na kila mmoja anafahamu kuna nchi inaitwa Tanzania, anakotoka mshambuliaji  Samatta.

Samatta ni kioo nje ya mipaka ya Tanzania baada ya hivi karibuni kujiunga na klabu ya Konibklijke Racing Club Genk (KRC), ya Ubelgiji akitokea klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidomakrasi ya Congo (DRC).

Kwa kutambua mchango wa Samatta na baadhi ya wachezaji wengine wanaocheza nje ya nchi, hii ni orodha yao wanaopeperusha bendera ya nchi.

Samatta

Ndiyo nahodha wa Taifa Stars, akichukua kitambaa hicho kutoka kwa mkongwe, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Nyota huyo anasimama kama mchezaji mwenye mafanikio, ukilinganisha na nyota wengine nchini, kutokana na kufanya vema katika soka.

Samatta alianzia maisha yake ya soka katika klabu ya Kimbangulile FC, kisha Mbagala Market ambayo sasa ni African Lyon na baadaye Simba, amekuwa balozi wa wachezaji wa Tanzania nje ya nchi.

Mafanikio ya Samatta akiwa na TP Mazembe, yalimfanya aingie kwenye historia ya timu hiyo kama miongoni mwa wachezaji bora waliowahi kuichezea kwa mafanikio makubwa klabu hiyo ya Lubumbashi inayomilikiwa na Moise Katumbi.

Mrisho Ngassa

Nyota huyo anayecheza soka la kulipwa nchini Oman kwenye klabu ya Fanja ya nchini humo, baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini, ni miongoni mwa wachezaji bora nchini kwa miaka ya hivi karibuni ambao wamekuwa wakifanya vizuri kwenye klabu na timu ya taifa.

Ngassa aliyechipukia kisoka katika klabu ya Channel ya kwao Mwanza, kabla ya kusajiliwa Kagera Sugar na baadaye Yanga ni winga mahiri ambaye ana uwezo wa kufunga mabao.

Ubora wa Ngassa umemfanya kuwa miongoni mwa wachezaji waliowahi kuzichezea timu kubwa nchini za Yanga, Simba na Azam.

Nyota huyo aliwahi kufanya majaribio katika klabu ya West Ham ya England na Seattle Sounders ya Marekani, alishindwa kuishawishi kumsajili, huku mwaka 2012, akikataa kwenda kujiunga na El Merreikh ya Sudan, iliyokuwa ikimtaka bila kufanya majaribio.

Elius Maguli

Ni mshambuliaji wa zamani wa Simba na Stand United, ambaye kwasasa anakipiga katika timu ya, Dhofar SC ya Oman, amekuwa na mafanikio makubwa katika kikosi chake kipya kutokana na kupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.

Ni mchezaji ambaye ameweza kujipatia mafanikio makubwa katika michezo ya ndani akiwa katika timu zake na kufanikiwa kujipatia nafasi ya kucheza katika kikosi cha timu ya taifa 'Taifa Stars'.

Emily Mgeta

Mgeta ni kati ya wachezaji waliokuwa wakiunda timu ya vijana ya Simba B, iliyokuwa na wakali wengine Said Ndemla, Rashid Mkoko na Ibrahim Ajib.

Mchezaji huyo anayecheza nafasi ya ulinzi wa kushoto hivi sasa anacheza soka la kubwa katika klabu ya Neckasulm, inayoshiriki ligi daraja la tano nchini ya Ujerumani.

Mgeta alivyokuwa nchini alizitumikia timu za Simba B na baadaye kupandishwa A, Villa Squad na Polisi Morogoro ambayo hadi anaondoka kwenda Ujerumani alitokea timu hiyo.

Nyota huyo amezoea maisha ya Ujerumani baada ya kuwa na mtoto nchini humo ambaye amezaa na mmoja ya raia wa nchi hiyo.

Thomas Ulimwengu ‘Buffalo’

Pacha wa Samatta katika kikosi cha Stars. Nyota huyo amekataa kusaini mkataba mpya wa kuichezea TP Mazembe, msimu uliopita alikuwa na Samatta na kutengeneza muungano mzuri ulioipa mafanikio makubwa klabu hiyo.

Itaendelea...
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo