Tanzania yajipanga kutekeleza malengo ya SDGs


Suleiman Msuya

Profesa Makame Mbaraw
TANZANIA imesema ipo tayari kushirikiana na nchi mbalimbali kukuza sekta ya usafirishaji katika kutekeleza lengo la Mandeleo Endelevu Duniani (SDGs) kivitendo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wakati akiwasilisha hotuba yake mbele wa Wajumbe wa Mkutano wa Dunia kuhusu maendeleo endelevu katika sekta ua usafirishaji uliofanyika Ashgabat nchini Turkmestan.

Mbarawa alisema historia inaonesha kuwa usafiri ni njia ambayo inaendesha biashara, uchumi, kazi na maendeleo ya nchi, hivyo Tanzania imekuwa katika mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.

“Kwa sasa inabakia kuwa kiungo muhimu katika kuunganisha jamii na mipango endelevu, kwani usafiri wa kisasa unaleta ushindani na unatakiwa kuwa rafiki wa mazingira,” alisema.

Alisema sekta ya usafiri inaunganisha watu, huduma, uzalishaji na bidhaa kati ya nchi na nchi na dunia kwa ujumla.

Waziri Mbarawa alisema kuwa mwaka 2016 ni muhimu katika kufanikisha malengo ya SDGs 2030 kupitia usafiri katika kuondoa umasikini, kuboresha afya, miji na jamii.

Alisema jopo la wataalamu lilitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Oktoba 28 mwaka huu wakionesha mchango wa sekta ya usafirishaji katika kutekeleza SDG.

Waziri huyo alisema ili kufanikisha SDGs, Serikali inapaswa kuwekeza katika mfumo wa usafirishaji barabarani, majini, anga na maeneo yote yanayohusika ili kuongeza ubora wa maisha.

Alisema sekta ya usafiri inatakiwa kuwa tayari katika kuleta mapinduzi ya nne ya viwanda ili uzalishaji, huduma na teknolojia vinaenda kwa pamoja.

“Tunapaswa kutumia njia zote za usafirishaji kufanikisha usalama wa watu kusafirisha bidhaa, watu na mawasiliano kwa kanda zote,” alisema.

Waziri Mbarawa alimuwasilisha Rais John Magufuli katika mkutano huo uliondaliwa na UN katika kujadili nafasi ya sekta ya usafiri katika SDGs 2030.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo