Maoni ya bei mpya ya umeme yapitiwa


Emeresiana Athanas

MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), imeanza kupitia maoni ya wadau kuhusu maombi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kupandisha gharama ya umeme kwa asilimia 18.19 kuanzia mwakani.

Akuzungumza Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa Umeme Ewura, Godfrey Chibulunje alisema maoni hayo yalikamilika Novemba 25.

Alisema baada ya kuyapitia na kuyachambua, yatafikishwa kwenye Bodi ya Mamlaka hiyo na hatimaye kutoa uamuzi sahihi.  

"Novemba 25 ndiyo ilikuwa mwisho wa kukusanya maoni na tayari yameanza kupitiwa kisha yatafikishwa kwenye Bodi ya Ewura ili kutoa uamuzi," alisema.

Aliongeza kuwa uamuzi huo utatangazwa ndani ya mwezi huu ili kuhakikisha Januari bei mpya zinaanza kutumika.

Kwa mujibu wa Tanesco, maombi ya mabadiliko ya gharama yaliwasilishwa Ewura, kulingana na agizo la kubadilisha bei za umeme la mwaka huu lililoanza kutekelezwa Aprili.

Kwa mujibu wa agizo hilo bei hizo zinatumika hadi Desemba 31   na hivyo Januari zinatakiwa bei mpya za umeme kwa mujibu wa sheria.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo