Tamwa waja na siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia


Suleiman Msuya

Edda Sanga
CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa) kinaungana na mashirika yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili huo kwa wanawake na watoto hasa wa kike.

Hayo yalisemwa na mkurugenzi mtendaji, Edda Sanga, katika taarifa waliyoitoa kwenye vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam.

Alisema katika maadhimisho hayo ambayo yamebeba kauli mbiu ya “Funguka! Pinga Ukatili wa Kijinsia: Elimu Salama Kwa Wote”, inalenga kila mzazi, mlezi, ndugu na jamaa kwa kushirikiana na serikali katika kumlinda mtoto wa kike.

Sanga alisema Tamwa kupitia kituo chake cha usuluhishi (CRC), kinatoa huduma ya ushauri nasaha kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi na Newala Mkoani Mtwara.

Pia, alisema taasisi hiyo itaendelea kutumia vyombo vya habari kutoa elimu ya uelewa kwa jamii kuhusu vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.

“Tamwa inaamini kuwa ukatili wa kijinsia unaweza kupungua endapo wazazi, walezi, walimu, ndugu, jamaa wataona umuhimu wa kukemea vitendo hivyo kwa kushirikiana na serikali ili kuhakikisha vyombo vya maamuzi vinalivalia njuga suala hili,” alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo