TRAWU yapata uongozi mpya


Hussein Ndubikile

CHAMA cha Wafanyakazi wa Reli nchini (Trawu) kimepata safu mpya ya uongozi baada ya kukamilisha Mkutano Mkuu wa Uchaguzi uliofanyika Dodoma.

Akizungumza na JAMBO LEO jana, Makamu Mwenyekiti wa Trawu, Yusuph Mandai alisema wajumbe 89 walishiriki mkutano huo huku akibainisha kwamba nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho imechukuliwa na Lomitu ole Saitabau kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRL).

"Wajumbe 89 walipiga kura na kila mtu aliyechaguliwa alipata asilimia 50 ya kura zilizopigwa," alisema.

Alitaja wengine waliochaguliwa kuwa ni Katibu Mkuu, Christopher Kaziyo, Naibu Katibu Mkuu, Nashon Malyeri, Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake Taifa,Theresia Mahagatila na Makamu wake,Elizabeth Msemwa.

Alisisitiza kuwa safu ya uongozi iliyochaguliwa itatimiza majukumu yake kwa kufuata maadili na taratibu za kazi.

Aliongeza kuwa anafahamu kuwa wafanyakazi wa reli wana changamoto nyingi zinazowakabili hivyo watajipanga kuhakikisha zinapewa ufumbuzi.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo