Mawaziri wa afya EAC wapitisha sera ya afya


Mwandishi Wetu, Nairobi

Ummy Mwalim
MAWAZIRI wa afya wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wamepitishe sera ya afya na mwongozo na mkakati wa afya ya mama, mtoto na vijana.

Sera na mwongozo huo vimepitishwa katika kikao cha mawaziri hao kilichofanyika nchini Kenya ambapo Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu aliongoza kikao hicho.

Waziri Mwalimu alisema kupitia sera na muongozo huo makundi husika yatapata unafuu wa huduma za afya kwa kuwa zitasimamia utekelezaji wa mpango wa kuboresha na kuimarisha afya katika nchi wanachama.

“Sera hizi zitasimamia utekelezaji wa mipango ya kuboresha na kuimarisha afya katika nchi wanachama wa jumuiya kwa utaratibu unaofanana,” alisema.

Alisema mkutano huo wa mawaziri pia ulichambua na kupitia taarifa ya makatibu wakuu wa wizara zao ambapo ulieleza kuridhishwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa maagizo ya mawaziri wa afya ikiwemo kuanzishwa kwa mpango wa pamoja wa kusimamia dawa, mpango wa pamoja wa kukagua vyuo vikuu vya afya pamoja na mpango wa pamoja wa huduma za ukimwi/VVU.

“Taarifa ya ukaguzi wa vyuo vikuu vya afya vya Tanzania itawasilishwa katika kikao cha 14 cha mawaziri wa afya wa EAC kitakachofanyika Burund Machi, mwakani,” alisema.

Mwenyekiti huyo wa mkutano aliwataka mawaziri wenzake kutekeleza maamuzi waliyokubaliana katika mkutano huo ili kutimiza kwa vitendo matarajio ya wananchi wa EAC kuwa na afya bora.

“Mkutano huo ulitanguliwa na kikao cha wataalam na kikao cha makatibu wakuu wa wizara za afya katika nchi wanachama vilifanyika kuanzia Novemba 14 hadi 17, mwaka huu,” alisema.

Mkutano huo ulihudhuriwa na mawaziri wa afya wa Kenya, Burundi, Uganda pamoja na Mwakilishi wa Waziri wa Afya wa Rwanda.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo