Mwakyembe alia na wasiosaini Itifaki


Mery Kitosio, Arusha

Dk Harrison Mwakyembe
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe, ameeleza kusikitishwa na baadhi ya nchi za Afrika ambazo hazijasaini mkataba wa Itifaki wa  kuanzishwa Mahakama ya Haki za Binadamu akieleza kuwa kitendo hicho kinawanyima Watanzania fursa ya kupata haki.

Alisema kati ya nchi 54 za Afrika, ni 30 pekee ndizo zilizosaini Itifaki hiyo.

Alisema hayo juzi wakati akizungumza kwenye sherehe ya miaka 10 ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Haki za Binadamu jijini hapa.

Alisema katika kipindi hicho, wamepata mafanikio makubwa, lakini bado anasikitishwa na nchi ambazo hazijakubali kusaini.

“Kati ya nchi 54 za Afrika ni 30 tu zilizokubali kusaini Itifaki, lakini  naona hii inatokana na utashi wa kisiasa maana mbona nchi ambazo zilikubali ikiwamo Tanzania hazijapasuka vipande ziko tu vizuri?

“Bado sijaelewa sababu za nchi hizo kukataa Itifaki hiyo. Naziomba  ambazo hazijakubali zikubali ilikusudi hata wananchi wao wawe na uhuru wa kupeleka kesi zao mahakamani,” alisema Dk Mwakyembe.

Alisema pamoja na Tanzania kuongoza kuwa na kesi nyingi za kulaumiwa, bado ipo kwenye moja ya nchi zilizokubali kusaini Itifaki hiyo ingawa bado ipo katika kipengele cha kuwezesha wananchi mmoja mmoja kupeleka kesi zao mahakamani hapo.

Jaji mstaafu wa Mahakama ya Haki za Binadamu, Jaji Augustino Ramadhani alisema ni jukumu la Serikali ya Tanzania kujenga Mahakama eneo la Laki Laki, Kisongo, kwani ni kubwa na linakidhi mahitaji ya kujengwa Mahakama hiyo.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo