Makonda akata mirija ya ‘wapiga dili’


Salha Mohamed

Paul Makonda
MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepiga marufuku baadhi ya idara katika halmashauri za jiji kupewa fedha mara kwa mara huku wahusika wanaotoa fedha hizo wakitegemea kupata asilimia kadhaa.

Makonda ametoa onyo hilo wakati akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Ubungo kupitia ziara yake ya siku kumi mkoani humo yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero na changamoto za wananchi ili kuzitolea ufafanuzi.

Alisema zipo idara katika halmashauri ambazo hupewa fedha mara kwa mara sababu ya kuwa na uhakika wa ulaji.

"Kuna baadhi ya idara hudai fedha hizo zimepelekwa kwenye mradi wa maji au ujenzi wa barabara kwa madai kwamba ni barabara muhimu kumbe wahusika wanamkataba na wakandarasi ya kwamba akipata fedha za malipo asilimia fulani atoe kwao," alisema.

Kutokana na hali hiyo Makonda alisema anataka watu waadilifu na wanaowajibika na kueleza kuwa ni vyema kuwatambua wanaofanya kazi na kumsaidia Rais pamoja na kuwatambua wavivu na mizigo wanaokula fedha za mshahara bila kufanya kazi.

Makonda alisema: "Ifikie wakati watumishi hao katika kujiletea matokeo mazuri wajiulize kwamba wamehudumia watu wangapi katika ofisi zao na si wamenufaika vipi na ofisi hizo," alisema.

Aidha aliwataka watumishi wa wilaya hiyo mpya ya Ubungo kufanya kazi kwa uadilifu ili wananchi watamani kwenda katika manispaa hiyo kupata huduma.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo