Watakiwa kufanya kuhudumia vizuri wagonjwa


Mwandishi Wetu

Profesa Mohamed Bakari
MGANGA Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Bakari, ametaka watoa huduma za afya nchini kufanya kazi kwa bidii na kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

Profesa Bakari alitoa kauli hiyo wakati akifungua kongamano la siku tatu la Chama cha Wafiziotherapia Tanzania (APTA) juzi Dar es Salaam.

“Mnatakiwa kuwa na nidhamu na kuhudumia vizuri wagonjwa. Fanyeni kazi kwa bidii kwani nchini kuna mabadiliko makubwa ya kiutendaji,” alisema Profesa Bakari.

Aliwataka kuzingatia maadili ya kazi kwani Serikali ya sasa inataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza uzalishaji na kutoa huduma bora katika maeneo yao ya kazi.

Kongamano hilo lilikutanisha wataalamu wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo