Mufti: Fanyeni usafi siku ya Maulid


Jemah Makamba

Shehe Mkuu Abubakar Zubeir
MUFTI wa Tanzania, Shehe Mkuu Abubakar Zubeir, ametaka Waislamu nchini kuadhimisha siku ya Maulid kwa kufanya usafi, kupanda miti na kuchangia damu.

Alisema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Dar es Salaam jana.
                                              
Mufti Zubeir alisema Maulid ya mwaka huu yatasomwa usiku wa Desemba 11, ambapo kitaifa yatafanyika Singida, wilayani Iramba na siku inayofuata Desemba 12 Batraza la Maulid litasomwa kuanzia saa nne asubuhi Shelui.

Alitumia fursa hiyo kuwataka Waislamu nnchini watumie siku hiyo kuonesha vitendo vyema na kufanya usafi kwenye mitaa yao na kuchangia damu ili kusaidia wenye uhitaji wa damu.

Aidha, alisema ataongoza usafi kufurahia siku hiyo ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) kwa kuwa Uislamu ni usafi.  

Alisema yeye na familia yake watafanya usafi mtaani kwake Mikocheni na kuchangia utoaji damu.

Aliwataka Waislamu kutojiingiza kwenye makundi ya ugaidi kwani Uislamu si ugaidi, hivyo kuwasihi waachane na tabia hizo.

Alisema walitarajia mgeni rasmi awe Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa lakini bado hawajajibiwa maombi yao, hivyo wakishajibiwa watu watajulishwa kabla ya siku yenyewe.

Aliwataka viongozi wa Bakwata kusimamia na kuhimiza amani ya nchi  bila kuvumilia wenye tabia za kuharibu amani na utulivu wa nchi.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo