Mahakama kumaliza mvutano wa maiti


Grace Gurisha

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo inatarajia kutoa uamuzi wa madai ya mwili wa marehemu Ernest Materego uzikwe wapi baada ya kutokea mvutano mkubwa wa ndugu wa marehemu.

Uamuzi huo wa Mahakama hiyo unatokana na mvutano wa ndugu wa marehemu hao ambao wengine wanataka ndugu yao azikwe Dar es Salaam huku wengine wakitaka akazikwe Bunda, Mara.

Mgogoro huo uliibuka Novemba 19 Materego alipofariki dunia, na   mtoto wa marehemu, mke na mdogo wa marehemu, ambapo kila mmoja alikuwa na uamuzi wake, ndipo walipoamua kukimbilia mahakamani.

Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Thomas Simba, baada ya kushindwa kutoa uamuzi huo jana kutokana na kuwapo vitu vingi ambavyo alitakiwa avisome ili atoe uamuzi.

Hakimu Simba alifikia uamuzi huo, baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, ambapo wadai walitaka kuzika Dar es Salaam kwa sababu ndiko marehemu alikoishi uhai wake wote wa miaka 70.

Hata hivyo, mdaiwa akijibu madai hayo, alidai marehemu alikuwa akiishi pia Bunda, hivyo anatakiwa kuzikwa huko na si Dar es Salaam, ambapo waliiomba Mahakama itoe amri ya muda, mwili usizikwe hadi madai yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Wadai katika kesi hiyo ni Edwin Materego, ambaye ni mtoto wa marehemu na mke wa marehemu, Joyce Materego.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo