Mvua yasababisha kizaazaa Dar


Leonce Zimbandu

MVUA zinazonyesha Dar es Salaam zimesababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara, madaraja na baadhi ya huduma za kijamii kusimama katika maeneo mbaloimbali.

JAMBO LEO jana ilitembelea Buguruni Malapa, bonde la Mto Msimbazi, barabara ya Kawawa, Mikocheni, Kawe na kushuhudia maji barabarani, mitaroni na baadhi ya maduka kufungwa na wananchi kushindwa kuendelea na biashara zao.

Wakati mvua hiyo ikinyesha abiria  walijificha kwenye vituo vya daladala, huku baadhi wakishindwa kupanda wala kushuka vituoni  kutokana na maji kujaa barabarani.

Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya wakazi wa maeneo yaliyoathirika, walisema mvua hiyo inaweza sababisha maafa hasa kwa wakazi wa mabondeni ambao walishindwa kuchukua hatua ya kuhama.

Mkazi wa Buguruni, John Mkalamba alisema huu ni msimu wa mvua, hivyo wanaoishi maeneo hatarishi wanapaswa kuchukua hadhari na kuondoka.

Alisema mvua ya siku moja tu imesababisha madhara haieleweki kama itaendelea kunyeshwa kwa kiwango gani, kwani hali ya miundombinu si nzuri.

“Huu ni msimu wa mvua hivyo kutokana na miundombinu mibovu mafuriko yanaweza kutokea, kwani mvua ya siku moja baadhi ya magari yameshindwa kutembea barabarani,” alisema.

Mwelekeo wa mvua za vuli katika kipindi cha Novemba, kulitarajiwa na   upungufu wa mvua katika maeneo mengi ya nchi katika kipindi hicho.

Taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilisema maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki na maeneo ya mkoa wa Tabora mvua zilitarajiwa kunyesha katika wiki ya tatu za Novemba.

Iliendelea kusema kuwa mvua za wastani hadi chini ya wastani zilitarajiwa katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria na  mvua za chini ya wastani katika maeneo mengine ya nchi.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo