Shule yafungwa bila mitihani


Warioba Igombe, Morogoro

Msamvu, Morogoro
WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Mtoni Moro mkoani hapa wamefunga shule bila kufanya mitihani ya kumaliza muhula, huku mwalimu mkuu wa shule hiyo, Mhina Mlimbo akituhumiwa kwa ubadhilifu wa fedha zitokanazo na ada ya wanafunzi.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa shule hiyo ilifungwa Oktoba 15 kutokana na kukosa fedha za kujiendesha. Chanzo hicho cha habari kimeeleza kuwa mbali na ubadhirifu uliosababisha walimu kutolipwa misharaha yao tangu Januari mwaka huu, shule hiyo pia haina bodi, Bendera ya Taifa, wala picha ya Rais.

Hata hivyo, mwalimu Mlimbo alikanusha tuhuma kwamba anahusika na ufujaji wa fedha na kubainisha kuwa taarifa hizo zinaenezwa na mmoja wa walimu ambaye amefukuzwa shuleni hapo baada ya kutaka kumsaidia mwanafunzi mtihani wa taifa.

Kuhusu kufunga shule mapema mwalimu huyo alisema shule hiyo ilifungwa mapema ili kupisha mitihani ya taifa kwa kidato cha nne ili wanafunzi waweze kufanya mtihani katika hali ya utulivu bila bugudha yoyote.

Mkurugenzi wa shule hiyo, Bernadeta Masuka amekiri kupokea tuhuma hizo na kueleza kuwa kwa sasa hawezi kutoa tamko lolote, kwani afya yake siyo nzuri na kwamba itakapoimalika atashughulikia changamoto zote za shule hiyo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo