Lugone: Lipumba ni bidhaa ya CCM


Suleiman Msuya

Profesa Ibrahim Lipumba
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema dhambi ya usaliti inamtesa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.

Aidha, CUF imesema Lipumba amezoea na ameshaonja ladha ya kutumika hali ambayo hawezi kuiacha kwani inamfaidisha.

Kauli hiyo ya CUF inakuja ikiwa ni siku moja baada ya Lipumba kuibuka na kumjibu Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kumtaka afuate taratibu ili kufanikisha mikutano yake.

Taarifa iliyotolewa na Ofisa Mawasiliano na Uchaguzi CUF Taifa, Abdulrahman Lugone, ilisema kuwa kiongozi huyo amekuwa akikisaliti chama hicho kwa muda mrefu ikiwamo, mwaka 2010 kwa kumsaidia mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Rais mstaafu Jakaya Kikwete kushinda.

“Mwaka 2015 alipoona hawezi kugombea urais akajua wanunuzi wataona hana thamani, akaona njia ni kujitoa kwenye chama ili wanachama wavurugike ambapo mpango wake ulifeli vibaya kwani CUF ni taasisi,” alisema.

“Wanunuzi wake, CCM, waanze kutafuta bidhaa nyingine kwa sababu CUF ilishamalizana naye. Waendelee kumpa ulinzi wa Polisi, wampigie saluti, wampe uenyekiti wa chama kwa nguvu ya dola yote hayo hayataihamisha CUF kwenye ajenda zake katika kuwapigania Watanzania na Wazanzibari kwa ujumla,” alisema.

Lugone alisema ni vema jamii ikajiuliza maswali ya msingi  ni mahali gani duniani kiongozi wa juu wa taasisi kubwa kama CUF ambaye aliwahi kuandika barua ya kujiuzulu na kuiacha ofisi yake kwa muda wa miezi kumi akarudi kwa mfumo huo wa Lipumba.

Alisema CUF ilichagua kiongozi mbadala wa nafasi hiyo hiyo, hivyo wao hawapo tayari kuona utaratibu wa chama ukikiukwa kwa maslahi ya mtu mmoja.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo