Kuhitimu chuo Hombolo sasa mpaka ‘kwata’


John Banda, Dodoma

George Simbachawene
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi George Simbachawene amesema kuwa kila mhitimu wa Chuo cha Serikali za Mitaa anatakiwa kupewa mafunzo maalumu ya ukakamavu ili kuweza kukabiliana na wahalifu wanapoanza kufanya kazi na kujitegemea.

Waziri huyo aliyasema hayo wakati alipokuwa akiwahutubia wahitimu 700 katika mahafali ya nane ya chuo hicho kilichopo katika Kata ya Homboro, manispaa ya Dodoma mwishoni mwa juma.

Waziri huyo alisema iko haja kwa wanafunzi wanaohitimu chuoni hapo kupata mafunzo ya ukakamavu kwa sababu wakishaajiriwa wataongoza askari wa akiba au waliopo katika kupambana na wala rushwa, majambazi na wakati mwingine watakiwa kutoa maelekezo ya namna yakuwakata watuhumiwa wa makosa ya jinai.

 “Kutokana na mfumo wa kazi mnaokwenda kuifanya ni vema mkapata mafunzo yanayoendana na maswala ya usalama pia ukakamavu, mjue hata ABC za silaha ili atakapokuwa amesikia imepigwa ajue namna ya kukabiliana na walengwa,

Wiki za mwisho waje JKT kuwapa mafunzo maalumu ili wakitoka wawe na ukakamavu na mbinu za kutosha za usalama ili wanapokuwa kazini waweze kupambana na wahalifu hata kama wanatumia silaha na wale waliovunja sheria kwa kufanya makosa ya jinai”, alisema

Aidha alisema wahitimu hao ambao wanaandaliwa kwa ajili ya kuwa watendaji wa kata na vijiji ambao pia wanakuwa wenyeviti wa kamati za shule hivyo si watu wa kawaida hivyo ni vema wakapata ujuzi huo ili waweze kufanya ueledi wao.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo