Serikali iboreshe miundombinu



Mary Mtuka

Edda Sanga
MTANDAO wa wadau katika asasi za kiraia umeiomba  Serikali kuboresha miundombinu ya barabara zinazojengwa kuzingatia matumizi ya watumiaji wote na kuzifanya salama kwa wote.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa maadhimisho wa siku ya kuwakumbuka wahanga wa ajali za barabarani, ambayo hufanyika Novemba 20 kila mwaka.

Akizungumza Dar es Salaam jana katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Chama Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Edda Sanga alisema Serikali inawajibika kuzifanya barabarani kuwa sehemu salama kwa kila mmoja.

Alisema ajali za barabarani zimekuwa na athari nyingi hapa nchini kiuchumi na kijamii, kwani takwimu zinaonesha kuwa takribani watu milioni 1.24 duniani hufariki kila mwaka kutokana na ajali.

"Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusiyo usalama barabarani Tanzania, kama ilivyo ratibiwa na Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (Tawla) tunaomba serikali na watunga sheria kuifanyia maboresho ya sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973," alisema.

Mkurugenzi huyo alisema maeneo ya maboresho ya sheria hiyo ni pamoja na mwendokasi ambao umekuwa sababu  kubwa ya ajali zinazogharimu uhai wa watu wengi.

Mkurugenzi wa Programu kutoka Tawla Nasieku Kisambu alisema katika kuadhimisha siku hiyo wanaomba kuwepo kwa usimamizi wa usalama wa vyombo vya moto vinavyo ingia nchini, ili kujua kama vitamlinda mtumiaji pindi inapotokea ajali.

Pia alisema Serikali inapaswa kuwa na magari ya kutoa hudumia ya kwanza baada ya ajali kutokea kwani ni moja ya changamoto nchini.

Kwa upande wake mmoja wa wahanga wa ajali Salumu Haji alitumia fursa hiyo kushukuru msaada alioupata kutoka  Tamwa tangu alipo pata ajali mwaka 2012.

"Nilipata ajali na nikapoteza mguu wangu mmoja na kusababisha kukimbiwa na mke wangu na kuniacha na watoto wa wawili wanao nitegemea hadi  " alisema.

Hata hivyo alisema anaiomba serikali na watu wengine kumsaidia kuweza kujiajiri ili kuweza kuwahudumia watoto wake, hata ikiwezakana kupata bajaji.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo