Taasisi ya Kikwete yaokoa milioni 850/-


Mwandishi Wetu

TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeokoa Sh milioni 580 ambazo Serikali ingetumia kupeleka wagonjwa 20 wa moyo India kwa ajili ya matibabu kwa kila mgonjwa kutumia Sh milioni 29.

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alisema hayo jana wakati akielezea upasuaji wa moyo wanaoufanya sasa kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa moyo kutoka Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Australia.

Profesa Janabi aliongeza kuwa upasuaji huo wa wagonjwa unakwenda sambamba na utoaji elimu kwa wataalamu wa ndani wakiwamo madaktari, wauguzi, wagavi na mafundi wanaohusika na utengenezaji mashine za  matibabu.

“Idadi ya wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji ambao utachukua muda wa siku sita ni 20 kati yao watoto ni 15 na watu wazima ni watano,” alisema.

Alitaja gharama wanazolipa wagonjwa hao kuwa ni Sh  laki tano za vipimo vya maabara kwa wenye uwezo wa kulipia, kwa wasio na uwezo wanalipiwa na Serikali, Rotary Club Dar es Salaam na Bahari Beach na BAPS  Charity na wagonjwa ambao ni wanachama wa Bima ya Afya wanalipiwa na bima zao.

Alisema: “Wagonjwa wanaotumia kadi za Bima ya Afya ni wachache,  nawashauri wananchi wajiunge na Bima ya Afya kwani gharama za matibabu ni kubwa na tunakoelekea watu hawatalipa nasi kama taasisi hatuwezi kufanya upasuaji bure, kwani tunahitaji kununua vifaatiba ili kutoa huduma nzuri.”

Alitaja changamoto wanazikabiliana nazo kuwa ni damu kwani wanatumia chupa sita hadi nane kwa mgonjwa mmoja kutokana na wagonjwa kukosa damu ya kutosha.

Tangu mwaka jana, Taasisi imekuwa ikiweka kambi ya  matibabu ya moyo kwa kushirikiana na taasisi za kimataifa zikiwamo za OHI, Okoa Moyo wa Mtoto (SACH) na Mending Kids (MKI) ya Marekani na madaktari wa nchi hizo wamekuwa wakija na vifaatiba  na kijigharimia nauli.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo