Ajuza mwenye ulamevu abakwa


Frankius Cleophace, Tarime


MWANAMKE mwenye umri wa miaka 60 ambaye ana ulemavu wa viungo mkazi wa kijiji cha Kemakorere kata ya Nyarero wilayani hapa anadaiwa kubakwa Novemba 15 saa 5 usiku na Wambura Nyaraita ‘Oyesu’ mwenye umri wa miaka kati ya 25 na 30 mkazi wa kijiji hicho.

Baada ya kitendo hicho, Oyesu alitokomea kusikojulikana na jamii kuiomba Serikali kuingilia kati ili kijana huyo akamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria ili liwe fundisho kwa wengine.

JAMBOLEO ilizungumza na mwathirika huyo ambaye jina lake linahifadhiwa lakini mwenye ulemavu wa miguu na mkono aliyedai kuwa siku hiyo akiwa amelala alisikia kijana huyo anamfuata kitandani na kumtisha huku akimwomba fedha na kisha kumbaka.

“Nilikuwa nimelala nikasikia kijana huyo anaingia chumbani mwangu ambamo nalala peke yangu, akaniuliza kwa nini nalala na nguo na akaniuliza vitu vitatu; pesa, mwili wangu na roho, kuwa nimpe kimojawapo, nilivua nguo akalala na mimi kuanzia saa tano usiku mpaka saa tisa alfajiri … niliogopa kupiga kelele,” alisema bibi huyo.

Alimwomba Rais John Magufuli asikie kilio chake hicho na kumsaidia usafiri kwani pamoja na kuwa mlemavu hana baiskeli ya magurudumu matatu kwa ajili ya kutembelea ili kupata huduma za kijamii licha ya kutendewa unyama huo.

Motende Marwa, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, alithibitisha tukio hilo huku akisema jamii haina budi kulaani kitendo hicho, na kuomba Jeshi la Polisi kutofumbia macho suala hilo, ili kuhakikisha kijana huyo anasakwa kokote aliko na kutiwa nguvuni.

Diwani wa Nyarero, Marwa Mhabas alilaani kitendo hicho huku akisema katika kata yake ni mara ya kwanza kutokea.

“Hiki kitendo cha kinyama katika kata yangu ni cha kwanza nakilaani na kuahidi kutoa ushirikiano kuhakikisha kijana huyu anatiwa nguvuni, kwa sababu anajulikana na ni wa kijijini hapa,” alisema Diwani huyo.

Thomas Joseph, Msaidizi wa Kisheria wa Kata hiyo kutoka shirika la North Mara Paralegal pamoja na ndugu jamaa kwa ujumla wakizungumzia ukatili huo waliiomba Serikali kuingilia kati.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo