Ujerumani yaipa EAC bilioni 60/-


Mery Kitosio, Arusha

SERIKALI ya Ujerumani kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) imetoa msaada wa euro milioni 30 (Sh bilioni 60)  kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ili kutoa chanjo kwa watoto wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.

Mbali na msaada huo wa chanjo, Serikali pia imetoa euro milioni 10 kwa ajili ya kuwekeza kwenye maabara ya watoto ili kuhakikisha magonjwa ya watoto yanatokomezwa kwa wakati.

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mkataba wa fedha hizo katika makao makuu ya jumuiya hiyo juzi, Balozi wa Ujerumani ambae pia ni Mwakilishi wa Benki hiyo, Egon Kochanke alisema kutolewa kwa msaada huo wa fedha kutapunguza magonjwa ya watoto.

Alisema fedha hizo zitahudumia watoto wote wa Jumuiya kwa kuwapa chanjo za kukinga magonjwa na pia kupunguza matatizo kwenye sekta ya afya ya upungufu wa dawa hasa za watoto.

"Serikali yetu ya Ujerumani leo hii tumesaini mkataba na Jumuiya hii ya Afrika Mashariki na tumetoa Sh milioni  60 za maabara ili kutoa chanjo ya watoto kwenye sekta ya afya.

“Lengo letu ni kuhakikisha wanapata huduma za kiafya, kuanzia wanapozaliwa si watoto wanapelekwa kupata chanjo wanaambiwa zimekwisha," alisema.

Akielezea msaada wa fedha hizo za maabara ya watoto, alieleza kuwa kuwepo kwa maabara hiyo kutapunguza magonjwa yanayopata watoto, kwani itakuwa ni maabara ambayo ni maalumu tu kwa ajili ya kupambana na udhibiti wa magonjwa ya watoto wa nchi za Jumuiya.

Akizungumza baada ya kumaliza kusaini mkataba wa fedha hizo, Katibu Mkuu wa EAC, Liberat Mfumukeko aliishukuru Serikali ya Ujerumani kwa misaada hiyo, ambayo wamekuwa wakiitoa kwa Jumuiya hiyo na kusema kuwa itapunguza changamoto za afya hasa kukabiliana na vifo vya watoto.

Mfumumeko alisema fedha hizo ambazo zinalenga kusaidia watoto wote wa Jumuiya atahakikisha zinafikia walengwa, huku akiangalia zaidi zile nchi ambazo zina mahitaji makubwa ya kutibu chanjo hizo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo