Mbaroni kwa kumlawiti mwanafunzi

Joyce Anael, Hai

MKAZI wa Jijini Arusha aliyefahamika kwa jina la Elfosoo Munisi (38), anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16.

Imedaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alimlawiti mwanafunzi huyo, baada ya kumpatia kitu kinachohisiwa kuwa dawa za kulevya.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro
Koka Moita, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 21 mwaka huu majira ya saa 11:30 jioni katika maeneo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wilayani Hai mkoani humo.

Alisema Polisi inamshikilia mtu huyo na kuendelea na uchunguzi ili kubaini ukweli kuhusu tukio hilo alilomfanyia mwanafunzi wa kidato cha tatu anayesoma katika shule ya sekondari KIA wilayani humo.

Kaimu kamanda huyo aliendelea kusema kuwa awali kabla ya kijana huyo kufanyiwa kitendo hicho akiwa shuleni kwake alikutana na mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa ni mwalimu Kennedy ambaye walipeana namba za simu kwa mawasiliano.

Alisema simu siku ya tukio waliwasiliana na kukubaliana kukutana katika eneo la KIA na baada ya kuonana mwanafunzi huyo aliwekewa kilevi asichokifahamu na kisha kulawitiwa na mtu huyo anayedai kuwa ni mwalimu.

Aidha alisema Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa hizo lilichukua hatua ya kumpeleka kijana huyo hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanaro ya Mawezi na kubaini ukweli kuwa alilawitiwa.

Alisema baada ya mahojiano ya kina na kijana huyo Polisi ilimkamata mtuhumiwa huyo Novemba 26 mwaka huu na kwamba bado anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.

Kamanda Koka alisema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika iwapo itathibitika kama kweli alimfanyia kitendo hicho kijana huyo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo