Kampuni yaahidi kukamilisha barabara mapema


Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya ujenzi ya China (CCECC), inayojenga barabara ya Magole-Turiani mkoani Morogoro, imeahidi kukamilisha ujenzi huo mapema, huku ikiiomba Serikali iiunge mkono kufanikisha azma hiyo kwa kutoa fedha kwa wakati.

Ahadi hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa Asasi ya Urafiki wa Tanzania na China, Joseph Kahama, aliyeeleza kwamba siku za nyuma Serikali ilikuwa ikichelewa kutoa fedha za ujenzi wa miradi na kusababisha kusimama mara kwa mara.

“Nina matumaini makubwa ya ujenzi kukamilika kwa muda mwafaka, kuna mawasilianao ya mara kwa mara kati yetu na TanRoads, pia tayari Serikali imetoa Sh bilioni 41.8, kati ya Sh bilioni 66.7 zinazotarajiwa kujenga barabara hii,” alisema Kahama.

Alisema hakuna siku mpya ya kukamilisha kazi hiyo iliyokubaliwa na kwamba wafanyakazi wana ari ya kazi ya kukamilisha mradi mapema, iwapo Serikali itatoa fedha muda mwafaka, lakini kasi ya ujenzi itadorora kama fedha hazitapatikana kwa wakati.

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe amekaririwa katika vyombo vya habari akimhimiza mkandarasi huyo kukamilisha kazi kabla au ifikapo Septemba mwakani.

Kahama alisema Dk Kebwe alijionea hali halisi ya ujenzi wa barabara na kuhakikishiwa na Mhandisi Khatibu Khamis, kwamba kazi itakamilika muda mwafaka kwani hakuna tatizo la vifaa au wafanyakazi.

Barabara ya Mikumi-Mzina inaunganisha Tanga na mikoa ya Morogoro na Dodoma.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo