Wapentekoste wamwomba JPM awasuluhishe


Peter Akaro

Rais John Magufuli
UMOJA wa Maaskofu wa Kipentecoste Tanzania (UMKT) umetoa msimamo juu ya mgogoro kati yao na Baraza la Makanisa ya Kipentecoste Tanzania (CPCT) ukimwomba Rais John Magufuli na Askofu Sylvester Gamanywa kuingilia kati kabla ya kufikishana mahakamani.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa juzi na Mwenyekiti wa UMKT, Askofu Pius Ikongo ilieleza kuwa sheria inataka kabla ya madhehebu au taasisi za kidini kufikishana mahakamani, ni vizuri kutanguliwa na usuluhisho na wameshakwenda mahakamani kushauri hilo.  

“Hatukubaliani na kitendo cha kufutwa kwa Baraza  na kutumika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kulazimisha madhehebu ya kipentecoste kuwa wanachama wa CPCT,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Pia walipinga kitendo cha Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kijamii kulazimisha wateja wake wanaokwenda kwao kupata huduma za usajili kutambuliwa na CPCT kwanza na kulipa Sh 200,000 kuwa mwanachama.

“Hatukubaliani na uongozi wa CPCT kuwakataa na kuwaondoa maaskofu kwenye nafasi zote za uongozi kitaifa, kimikoa, kiwilaya na kuwaweka wachungaji kuwa viongozi na watatuzi wa migogoro ya madhehebu ya kipentecoste Tanzania,” ilisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo