Bima yaweka malengo ya trilioni 1/-


Suleiman Msuya

Israel Kamuzora
KAMISHNA wa Bima, Israel Kamuzora, amesema sekta ya bima imejiwekea malengo ya kukua kufikia uchumi wa Sh trilioni moja mwakani.

Kamuzora alisema hayo wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Miaka 50 ya Bima nchini, kwamba malengo hayo yatawezekana kama watafikisha elimu ya bima kwa wananchi wote.

Kamishna huyo alisema wana mikakati ya kukuza soko la bima kutoka zaidi ya Sh bilioni 400 za sasa hadi Sh trilioni moja mwakani.

“Tunajipanga kwa kila njia ili kufikia wananchi wengi ili kujua mambo ya bima nadhani tutafanikiwa,” alisema.

Kamishna huyo alisema mkutano huo wa bima wa mwaka unawapa fursa wadau kujadili mambo yaliyofanyika mwaka uliopita na kubaini kilichofanyika vizuri.

"Mtaji wa sekta hii kwa sasa ni zaidi ya Sh bilioni 450 fedha ambazo sekta hii imewekeza, lakini pato lake ni Sh bilioni 650 na tunatarajia mwakani kufika Sh trilioni moja," alisema.

Alisema jamii inapaswa kujua umuhimu wa bima na hata tetemeko lililotokea Kagera lisingeleta malumbano ya misaada kama wananchi wangekuwa wamejikatia bima.

Naibu Katibu Mkuu Utumishi, Suzan Mlawi akifungua mkutano huo, alisema wakati uchumi wa nchi ukikua, kumekuwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya bima katika sekta mbalimbali kama za viwanda, kilimo nakadhalika.

"Sekta hiyo imekuwa ikichangia kwa mwaka uchumi kwa asilimia 16, sekta pia imekuwa ikiondoa hatari ambayo wangeipata watu au wafanyabiashara katika maisha yao ya uwekezaji," alisema.

Alizitaja changamoto zinazoikabili sekta hiyo kuwa ni pamoja na masoko na  elimu finyu juu ya bima, ambapo alisema kampuni nyingi za bima zimelenga watu wa chini na si kampuni kubwa zinazochangia pato kubwa kwa Serikali.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo