Samia aushukia uongozi CDA


Joyce Kasiki, Dodoma

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameushukia utendaji mbovu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu ya Mji wa  Dodoma (CDA), akiitaka mamlaka hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza  na makundi  mbalimbali ya  Mji wa  Dodoma wakiwemo mama lishe, vikundi vya usafi wa mazingira na viongozi wa vyama ikiwa ni majumuisho ya ziara yake mkoani Dodoma.

Kauli hiyo ya Samia iliwafanya wadau waliokuwa wamekaa katika ukumbi huo kumshangilia kwa makofi mengi ambayo yalimfanya kiongozi huyo kuweka msisitizo akisema:

"Makofi haya yanaashiria matatizo ndani ya CDA, mnapaswa kuzungumza na kujirekebisha. Kama hamrekebishiki, wapo wafanyakazi wengi ambao wanaweza kufanya kazi vizuri zaidi."

Aliitaka CDA kwenda na kasi ya uongozi wa awamu ya tano lakini pia katika kipindi hiki ambacho Dodoma inatarajiwa kuwa jiji kutokana na ujio wa Makao Makuu.

Vile vile aliitaka Mamlaka hiyo kushirikiana vyema na Halmashauri zinazouzunguka mji wa Dodoma kuhakikisha unapanuka zaidi.


Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo