Wizara yatoa mwongozo kuhudumia makundi


Peter Akaro

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harison Mwakyembe
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imetoa tamko na mwongozo kuhusu utoaji huduma kwa makundi maalumu yaliyo hatarini kuambukiza na kuambukizwa Virusi Vya Ukimwi.

Tamko hilo linakuja baada ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harison Mwakyembe kueleza kuwapo asasi zisizo za serikali zinazounga mkono mapenzi ya jinsia moja kwa kusambaza vilainishi, vipeperushi na elimu kwa siri kwa kivuli cha kutoa afya kwa wanaoishi na VVU.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema Wizara yake iliwaita wadau wanaofanya kazi katika eneo la kupambana na Ukimwi ili kutoa mwongozo kwa asasi zote zinazotoa huduma kwa makundi maalumu.

“Kwanza ni Serikali kuendea kutoa huduma bora za kupambana na Ukimwi kwa kuzingatia viwango vya kimataifa, bila kudharau sheria, mila, taratibu na desturi za Tanzania.

“Pia tutaendelea kutoa huduma bila kubagua mtu kwa misingi ya dini, kabila, chama au fedha,” alisema.

Waziri alisistiza kuwa suala la kutoa huduma ya afya kwa makundi maalumu itambulike kwa ujumla si kwa wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

“Pia mdau anayetoa huduma za kupambana na virusi vya Ukimwi ana wajibu wa kuzingatia sheria za nchi, na kama mdau ni shirika lisilo la serikali ana wajibu wa kuzingatia sheria za mashirika yasiyo ya serikali ya kimataifa,” alisema.

Aliongeza kuwa huduma zinatolewa kwenye vituo vya afya kwa ajili ya makundi maalumu zitaendelea kwa makundi yote, isipokuwa wataendelea kuzuia huduma hiyo katika ngazi ya jamii.

“Maana yake shughuli za mashirika yasiyo ya  serikali kwenda kwenye jamii kugawa vilainishi na kutoa elimu tunazizuia kwa muda hadi utakapotolewa mwongozo,” alisema.

Alisema Mganga Mkuu wa Serikali ataongoza kazi ya kupanga wadau katika maeneo watakayofanya kazi nchi nzima.

“Asasi zote zinazotoa huduma ya afya ni lazima ziidhinishwe na halmashauri husika kabla ya kufanya kazi na asasi zisizo za kimataifa.

Aliongeza kuwa makundi yaliyo katika hatari zaidi ya kuambukiza na kuambukizwa Ukimwi ni wasichana na vijana walio katika umri wa balehe, walio katika mazingira hatarishi, watoto yatima, wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.

“Pia wapo wanawake wanaofanya ngono kinyume na maumbile, watumiaji wa dawa za kulevya, wanawake wanaofanya biashara ya ngono, wafungwa, wakimbizi, wafanyakazi wanaohama kila mara na wafanyakazi wa migodini,” alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo