Takukuru yaagizwa kuichunguza TAFAF


Leonce Zimbandu

Valentino Mlowola
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki ameagiza Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza watendaji Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf).

Akipokea ripoti ya utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Kunusuru Kaya Maskini katika Mtaa wa Mambo Leo B Kata ya Sandali, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam jana, Kairuki alisema baadhi ya watendaji hao wanatuhumiwa kwa kujinufaisha kwa rushwa wakati wa utekelezaji.

Mpango huo ulianza kuendeshwa kuanzia Julai 2015 hadi sasa lakini imebainika zipo kaya zimeingizwa kinyemela baada ya wahusika katika kaya hizo kutoa kamisheni kwa watendaji wa Tasaf.

Alisema mtaa huo ulikuwa na wanufaika 118 lakini kuna kaya 40 zilibainika kuingizwa bila kukidhi vigezo, hivyo zinapaswa kurejesha fedha hizo ili wanufaika wengine wapewe.

“Nahitaji Jeshi la Polisi na Takukuru wachukue hatua za haraka kuchunguza na iwapo itabainika rushwa hatua zichukuliwe mara moja,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaviva allisema watatekeleza agizo hilo la waziri kwa kuhakikisha vyombo vya dola katika Manispaa hiyo vinachukua hatua ya kuwakamata ili kuwahoji watuhumiwa.

“Kuanzia sasa naikabidhi kazi hiyo kwa Ocd wa Temeke na Afisa Takukuru Wilaya ya Temeke kushughulikia shuala hilo haraka kwa kuchukua majina ya wanufaika wa mpango huo,” alisema.

Awali Diwani wa kata hiyo, Wilbert Tarimo alisema kuwa wakazi wa kata hiyo wanakabiliwa na changamoto mbili, ikiwamo nyumba zao kuwekewa alama X na Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) bila taarifa.

Changamoto nyingine kukosa eneo la kujenga Kituo cha Afya na kisima cha maji kushindwa kukamili na kusababisha usumbufu wa maji katika eneo hilo.

Alisema kitendo cha kuwekewa X kinawafanya wakazi wa eneo hilo kuishi kwa wasiwasi kwa kuhofia kubomolewa, hivyo wanaiomba serikali kuwasaidia.

“Tunakuomba Waziri utusaidie kwa kuwa kila tunapofuatilia hatupati majibu, hivyo wananchi hao wanahitaji majibu,” alisema.

Akikijibu malalamiko hayo, Waziri Kairuki alisema ataandika barua mbili; moja kwa Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa na nyingine kwa waziri Kilimo, Mifugo na Uvuzi Dk. Charles Tizeba ili kushughulia changamoto hizo.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo