Kamati Kuu Chadema yakutana kimyakimya


Celina Mathew

KAMATI Kuu ya Chadema imekutana kwa saa mbili huku lengo la kukutana likifichwa.

Gazeti hili juzi lilishuhudia baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo akiwamo, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji.

Hata hivyo, habari kutoka Chadema zilieleza kuwa kukutana kwa viongozi hao ni kujipanga kwa ajili ya mkutano wa Kamati Kuu siku yoyote, huku ikielezwa kuwa ajenda zitakuwa ni pamoja na hali ya kisiasa na operesheni Ukuta.

Lowassa na Sumaye waliingia eneo hilo asubuhi na baadaye kufuatiwa na viongozi wengine.

Baada ya kumalizika kwa kikao hicho mchana gazeti hili lilimtafuta, msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene azungumzie mkutano huo, lakini akasema ni moja ya vikao vya kawaida vya chama.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo