Mkapa ahimiza utalii wa ndani


Jemah Makamba

Benjamin Mkapa
RAIS mstaafu Benjamin Mkapa ametaka Watanzania kujenga tabia ya kutembelea vivutio vya utalii nchini.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa filamu ya utalii ya Nshaba Ontwale Nyakijoga jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Rais Mkapa alisema vivutio vya utalii ni tunu ambayo Tanzania inazo, lakini wengi wa Watanzania hawana utaratibu wa kuzitembelea.

Mtunzi wa filamu hiyo, Profesa Wenceslaus Kilama alisema filamu hiyo yenye maana ya Naomba Nipeleke Nyakijoga, inaonesha vivutio vingi vya utalii vya mkoa wa Kagera ikiwamo misitu inayovutia ya Misenyi.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali wakiwamo wa kituo cha televisheni cha DSTV ambacho kilikuwa miongoni mwa waliofanikisha filamu hiyo.

Profesa Kilama aliwataka Watanzania wawe na kawaida ya kutembelea vivutio nchini na kwamba watakapoangalia filamu hiyo wataona uzuri wa Misenyi.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo