Waziri apendekeza bosi Posta asiwe mzawa


Celina Mathew

Profesa Makame Mbarawa
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amezindua Bodi mpya ya Shirika la Posta Tanzania (TPC) na kushauri Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo asiwe mzawa wa nchini.

Aliwataja watendaji hao kuwa ni Stella Mwanansao, Dk Ubena John, Dk Jasson Bagonza, Fatma Bakari, Khadija Shaaban na Leonard Kitoke.

Akizungumza Dar es Salaam juzi wakati akizindua Bodi mpya ya Shirika hilo yenye wajumbe sita huku nafasi ya Mtendaji Mkuu ikiwa bado wazi, alisema watu 207 walijitokeza kuwania nafasi hiyo.

Profesa Mbarawa alisema alikuwa akiuliza watu ili kupata maoni yao kuhusu mtendaji huyo atoke wapi na kwamba aliamua kuwa asiwe mzawa wa nchini, bali awe wa nje kutokana na kuwa kwa miaka mingi wazawa wamekuwa wakitumia shirika hilo vibaya.

"Tuliuliza Mtendaji Mkuu atoke wapi mimi nikaamua atoke nje ambaye hajui hata kupiga muhuri lakini suala kubwa azalishe fedha maana serikali inataka fedha na si kitu kingine lengo likiwa ni kuona shirika linasonga mbele kiuchumi," alisema.

Alisema endapo Mtendaji huyo atapatikana na kulichezea shirika kama waliopita, ataendelea kubadilisha hata kama atakuwa hajamaliza mwaka hadi apate kile anachokihitaji ambacho ni ukusanyaji mzuri wa mapato.

"Fedha zipo Posta tena nyingi, lakini hazionekani, haijafungwa mkono bali kulikuwa na watendaji wabovu kipindi kilichopita, ambapo mwaka jana kulitokea jambo ambalo halikuwa zuri la viwanja vitatu vya shirika kuuzwa kinyemela na baada ya kugundua tulifanyia kazi japo Bodi ilikuwa haijui," alisema.

Aliongeza kuwa katika shirika hilo kulikuwa na watu wanajifanya wajanja na kuahidi kuwa atahakikisha anawawajibisha, hivyo kuwataka kufikiria zaidi na kuachana na utendaji wa zamani kwa kutumia fursa zilizopo ili mafanikio yaweze kupatikana.

Aidha, aliahidi kulipa madeni ambayo TPC inaidai Serikali na kutoa mwaka mmoja kwa shirika hilo kuhakikisha linafungua kituo cha huduma kwa lengo la kufanya kazi kimaadili na kwa weledi.

Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Kanali mstaafu Dk Harun Kondo alisema kwa sasa shirika litakuwa na historia nzuri kutokana na kuwa wajumbe walioteuliwa ni watendakazi wazuri huku akikiri kuwa changamoto ya awali iliyokuwapo ilisababishwa na watendaji waliopita.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo