Mauritania kinara wa biashara Kusini mwa Afrika


Leonce Zimbandu

Rita Ramalho
BENKI ya Dunia imeitaja Mauritania kuongoza kufanya biashara za kimataifa kati ya nchi 49 zilizo kwenye ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, huku Kenya ikifuatia kwa kufanya vizuri kwa miaka miwili mfululizo.

Meneja wa Mradi wa Biashara wa Benki hiyo, Rita Ramalho aliitaja nchi hiyo kuongoza wakati wa kuzindua ripoti ya mwaka ya biashara iliyofanyika Dar es Salaam jana.

Alisema ripoti hiyo imezingatia viashiria vya kukua kwa uchumi katika nchi husika, ikiwamo Mauritania, ambayo imefanikiwa katika kulinda wawekezaji na kushughulikia utoaji wa vibali ya ujenzi kwa mtiririko kwa siku 156 tofauti na siku 183 za Ufaransa na 222 za Austria.

Alisema Kenya kwa mara ya pili mfululizo imefanikiwa kutatua tatizo la kupata idadi ya vizazi na vifo kwa kufuta ada ya uandikishaji na utoaji vyeti, kuanzisha mfumo wa habari kwa ajili ya kupata nishati ya umeme ili kupunguza muda wa mwingiliano.

"Bado jitihada za kufanya biashara kirafiki zinahitajika hasa kutokana na maboresho thabiti ya kiuchumi katika kanda mbalimbali, ingawa rekodi ya idadi ya mageuzi imeongezeka kwa asilimia 14 ikilinganishwa na mwaka jana, hivyo serikali zinapaswa kuweka msukumo katika mageuzi ya kiuchumi,” alisema.

Ripoti ya mwaka huu ilipokea kwa mara ya kwanza maombi ya Somalia na kufikisha nchi wanachama 190 ambayo kiuchumi hivi sasa inashika nafasi 190.

Ripoti ya biashara ya mwaka huu ilijikita kwenye viashiria vitatu ambavyo ni kuanzisha biashara, kusajili mali na kutekeleza mikataba iliyokubaliwa kimataifa kwa ajili ya kuboresha biashara na kuleta mageuzi ya kiuchumi.

Aidha, ripoti hiyo ilisema hatua za ziada zinahitajika kwa ajili ya kukomboa wanawake kwa kusajili biashara zao katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, zikiwamo Cameroon, Benin na Guinea-Bissau.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo