Raia 2 wa China kizimbani kwa utekaji, utesaji


Grace Gurisha

HATIMAYE raia watatu wa China wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakidaiwa kumteka na kumjeruhi mwenzao, Liu Hong na kumweka katika hatari ya kifo.

Watuhumiwa hao Chen Bao (34), dereva Wang Jian (37) na Zheng Pa Jin ‘Mr Ping’ (40) ambaye ni mfanyabiashara. Bao na Jian walikiri mashitaka huku Mr Ping akikana yote.

Akisoma hati ya mashitaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi Hellen Moshi alidai jana mbele ya Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha kuwa washitakiwa wanadaiwa kuteka na kujeruhi.

Moshi alidai kuwa Oktoba 21 raia hao wakiwa eneo la Palm Beach, Ilala walimteka Hong ambaye ni mwanamke kwa lengo la kumweka kumsababishia kifo.

Katika mashitaka ya pili, Moshi alidai kuwa siku hiyo hiyo na eneo hilo hilo, raia hao walimpiga Hong na kumsababishia majeraha mwilini.

Jian alikiri kumteka mwanamke huyo na kumjeruhi, huku Bao akimweleza hakimu kuwa alimchukua na kumweka hotelini, ila hakumteka kama inavyodaiwa na upande wa Jamhuri.

Mr Ping ambaye muda wote alionekana mkali, alikana kuhusika huku akitaka kujua hatima yake kwenye kesi hiyo kutokana na kwamba upelelezi haujakamilika.

Dhamana
Hata hivyo, kabla Mahakama haijapanga tarehe ya kutajwa kesi hiyo, Moshi alidai kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Ilala (RCO) aliwasilisha kipo kupinga dhamana ya raia hao kutokana na sababu maalumu saba.

Alidai kuwa kiapo hicho kiliapwa na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Salumu Ndalama, akieleza kuwa anajihusisha na upelelezi wa makosa ya jinai.

Na kwamba washitakiwa ni raia wa China na hawana taarifa za makazi yao nchini, hivyo hawastahili dhamana.

Moshi alidai kuwa Ndalama ana taarifa za kuaminika ambazo walizikusanya kupitia upelelezi wa kesi hiyo, kwamba washitakiwa hao na watuhumiwa wengine ambao hawajakamatwa, wanapanga kujihusisha na vitendo vya uhalifu Dar es Salaam ukiwamo utekaji.

Pia kiapo hicho kiliendelea kueleza kuwa zipo taarifa za kuaminika, kwamba washitakiwa na watuhumiwa ambao hawajakamatwa, wana mpango wa kumdhuru Hong kwa lengo la kupoteza ushahidi.

"Upelelezi bado unaendelea, wakipewa dhamana wanaweza kuingilia upelelezi na pia tuna taarifa za kuaminika kuwa Wachina wengine ambao ndugu yao alitekwa nyara, wanapanga kulipiza kisasi.

“Kwa hiyo ni kwa maslahi ya Jamhuri washitakiwa wabaki ndani hadi kesi itakapokwisha ili kulinda usalama wa Hong na raia hao," kilieleza kiapo hicho.

Washitakiwa hao ambao walikuwa wanatafsiriwa na mkalimani kwa kutokujua Kiingereza na Kiswahili, walielezwa na kujikuta wakipatwa kiwewe cha kutaka kujua hatima yao.

Hakimu Mkeha aliwauliza kama watawasilisha kiapo kinzani kujibu kiapo cha RCO, wakadai kuwa na mawakili wao kwa hiyo watalishugulikia hilo, lakini baadaye walionekana kukosa mwelekeo baada ya kukosekana mtu mwenye aarifa zao.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 14 siku ambayo upande wa washitakiwa utajibu hoja za RCO kupinga dhamana yao.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo