Bodi: Waliokosa mikopo wakate rufaa


Mwandishi Wetu

Abdul-Razaq Badru
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza siku 90 kuanzia jana ikitoa nafasi kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/17 kukata rufaa kwa njia ya mtandao, wakiona hawajaridhsihwa na matokeo ya upangaji uliotangazwa hivi karibuni.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru, ilisema Bodi imeanza kupokea rufaa hizo kwa njia ya mtandao kuanzia jana na itaendelea kupokea hadi Januari 31.

Serikali imetenga Sh bilioni 483 za mikopo kwa wanafunzi 119,012,  kati yao 93,295 ni wanaondelea na masomo na 25,717 ni wa mwaka wa kwanza. Hadi sasa, jumla ya wanafunzi 20,183 wa mwaka wa kwanza wamepata mikopo.

“Wanachotakiwa kufanya ni kulipa Sh 10,000 kwa njia ya M-Pesa na kuingia kwenye mtandao wetu wa http://olas.heslb.go.tz na kujaza fomu, kuichapa na kuiwasilisha kwa Ofisa Mikopo wa Chuo husika ambaye atawasilisha kwetu fomu zote za chuo kwa barua kwa ajili ya sisi kuzifanyia kazi,” alisema Badru.

Katika taarifa yake inayopatikana pia kwenye tovuti ya HESLB Badru aliongeza kuwa Bodi yake haitapokea wala kuzifanyia kazi fomu za rufaa zitazowasilishwa na wanafunzi bila kupitia kwa maofisa mikopo wa vyuo husika.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo