PPF na NSSF kujenga kiwanda cha sukari


Mery Kitosio, Arusha

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
MIFUKO ya hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF wameungana   kujenga kiwanda cha sukari eneo la Mkulazi mkoani Morogoro ili kukabiliana na tatizo la sukari nchini.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa sita wa wadau wa NSSF ulioanza jijini hapa jana, Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa alisema amefurahishwa na uamuzi wa taasisi hizo  kujenga kiwanda ili kukabiliana na tatizo hilo.

Majaliwa alisema kitendo kilichofanywa na mashirika hayo  ni cha  kuungwa mkono na mashirika mengine kuiunga mkono Serikali kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Alisema tathimini ya Tanzania ya kuwa na mahitaji ya zaidi ya tani 400,000 za sukari si sahii na hivyo kuiagiza Bodi ya Sukari kufanya tathimini mpya ya mahitaji ya sukari, ili viwanda viwe na tathimini ya kiwango cha uzalishaji.

"Nitoe mwito kwa kampuni na taasisi kuiga mfano wa NSSF na PPF kuunganisha nguvu katika utekelezaji wa agizo la kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda, ili kukuza uchumi wa  nchi yetu," alisema Majaliwa.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema kua shirika hilo limejizatiti kuwekeza kwenye sekta ya viwanda ili kuviwezesha kujiendesha kwa ufanisi na kuleta tija kwa wananchi.

Profesa alisema wameitika mwito wa Rais kuijenga Tanzania   ya viwanda kwa kuungana na PPF kujenga kiwanda hicho.

"Tunatarajia kujenga kiwanda hiki ambacho kitapunguza tatizo la sukari lakini pia kitatoa ajira zaidi ya 100,000 kwa Watanzania na hivyo kuongeza idadi ya wanachama," aliongeza Mkurugenzi.

Alihitimisha kwa kuwataka waajiri kuharakisha kuwasilisha makato ya waajiriwa wao kwa mujibu, kwani ucheleweshaji ni moja ya changamoto zinazowakabili.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo