Tanzania yazuia mazao kutoka Msumbiji


Richard Mwangulube, Arusha

TANZANIA imepiga marufuku uingizaji mazao ya migomba kutoka Msumbiji baada ya nchi hiyo kukumbwa na ugonjwa wa Panama.

Mbali na hatua hiyo pia Tanzania imeweka karantini nchi nzima kuzuia uingizaji wa mazao hayo.

Haya yalisemwa juzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florence Turuka katika hotuba yake wakati akifungua mkutano wa watalaamu wa afya ya mimea kutoka nchi za SADC na COMESA iliyosomwa kwa niaba yake na Cornelius Mkondo Mkurugenzi Msaidizi wa afya ya mimea.

Dk Turuka katika hotuba hiyo alisema Msumbiji inapakana kwa karibu sana na Tanzania hivyo si jambo jema wananchi kuruhusu migomba ama mazao ya migomba kutokana na ugonjwa huo hatari.

Katika kuhakikisha mazao ya migomba hayaingii nchini kutoka Msumbiji, Tanzania imeweka wataalamu wake wa mimea mpakani na nchi hiyo, viwanja wa ndege na maeneo yote muhimu ili kuimarisha ukaguzi

Kwa mujibu wa Dk Turuka, Tanzania kwa sasa haiwezi kusafirisha matunda kwenda Afrika Kusini kutokana na mdudu hatari anayeshambulia matunda.

Aliwambia washiriki wa mkutano huo kutoka nchi 15 za SADC na COMESA umuhimu wa kuwa na mikakati ya pamoja kukabiliana na magonjwa ya mimea katika ukanda huu wa Afrika.

Alisema hakuna nchi itakayokubali kununua matunda ya Tanzania ili kuepuka ugonjwa huo kuenea kwenye mataifa yao.




Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo