Benki ya Twiga taabani, yafungwa kwa wiki moja


Salha Mohamed

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imeichukua Benki ya Twiga na kusitisha huduma zake kwa wiki moja, baada ya kupungua mtaji na kuhatarisha usalama wa sekta ya fedha na amana za wateja.

Uamuzi huo wa BoT ni kwa mujibu wa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha Sheria namba 56(1)(g)(i) na 56(2)(a)-(d) ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006.

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu alisema jana kuwa kupungua kwa mtaji huo ni kinyume na matakwa ya sheria ya mabenki.

“Benki Kuu ya Tanzania imeisimamisha Bodi ya Wakurugenzi na uongozi wa Benki ya Twiga na kumteua Meneja Usimamizi atakayekuwa na jukumu la kusimamia shughuli za Benki ya Twiga kwa kipindi ambacho itakuwa chini ya usimamizi wa BoT,” alisema.

Alisema utoaji wa huduma za benki hiyo utasitishwa kwa   wiki moja ili kutoa nafasi ya kupanga shughuli za uendeshaji wa benki hiyo.

Profesa Ndulu aliongeza kuwa BoT haina haja ya kuisimamia benki hiyo kwa kipindi chote, kama atatokea mwekezaji anayeweza kuimiliki.

Alisema benki hiyo iliyokuwa chini ya Serikali kwa asilimia 100, mwaka juzi iliongeza mtaji baada ya BoT kuitaka kufanya hivyo, lakini bado hali haikuwa nzuri kutokana na madeni kuwa mengi na yasiyokusanyika.

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mabenki, Kenedi Nyoni alisema awali benki hiyo ilikuwa na mtaji wa Sh bilioni 7.5 ambapo wote uliisha na kubaki na mtaji chini ya sifuri wa hasi Sh bilioni 21.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo