UVCCM watetea umeya wa Sitta K’ndoni


Abraham Ntambara

Shaka Hamdu Shaka
UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umesema taratibu zilizotumika kumpata meya mpya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamini Sita kuwa zilikuwa sahihi na zilifuata miongozo ya kanuni, sheria na Katiba.

Kaimu Katibu Mkuu, Shaka Hamdu Shaka, alisema hayo wakati akizungumza mwishoni mwa juma na mwandishi wa habari hii.

“Tunaamini kwamba kulikuwa na wasimamizi wazuri wa sheria, kanuni na taratibu, hivyo ni imani yetu kwamba yote yalifanyika kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi,”alisema Shaka.

Shaka aliwataka wapinzani (Ukawa) wakubali kwamba walishindwa kadhalika wao bado ni wachanga kisiasa ikilinganishwa na CCM.

Aidha aliwataka Ukawa kuacha visingizio kwa kuwa walishindwa kihalali na malalamiko yao hayana mashiko.

Aliwataka kujua kuwa uchaguzi umemalizika hivyo baada ya uchaguzi kuna maisha mengine alisema pia wananchi wa Kinondoni washikamane na washirikiane kwa pamoja kuhakikisha wanaleta maendeleo kwa halimashauri yao.

Kwa upande mwingiene Shaka alisema Ushindi katika uchaguzi wa Kinondoni ni kiashiria kuwa kazi ndiyo imeanza ya kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa ujao wa mwaka 2019 na Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Alisema pia hiyo inamanisha kwamba tathimini ya uchaguzi mkuu uliopita ambapo walifanya makosa na kupelekea kupoteza baadhi ya Manispaa imekwishaanza kufanyiwa kazi na matunda yameshaanza kuonekana.

Shaka aliongeza kwamba wataendelea kujisahihisha kulingana na makosa waliyoyafanya ambapo hiyo ni mikakati ya kichama ili kuhakikisha kwamba hawarejei tena makosa ambayo yakawaghalimu.

Aidha alisema kutokana na utendaji kazi wa Rais Magufuli umeongeza imani kubwa ya wananchi kwa chama chao ambapo alibainisha kuwa watajitahidi kuwa karibu na wananchi hao ili iwe rahisi kupata ushindi bila upinzani katika uchaguzi ujao.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo