LAPF yawezekeza Sh bilioni 60 kwenye elimu


Joyce Kasiki, Dodoma

MFUKO wa Pensheni wa LAPF umefanya uwekezaji wa miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 60 katika sekta ya elimu mkoani Dodoma.

Uwekezaji huo umehusisha ujenzi wa nyumba 15, majengo mawili ya hosteli, viwanja vya michezo, sehemu ya kuogelea na barabara zenye urefu wa kilomita 5.4 katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo.

Aidha, LAPF katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), imejenga majengo mawili ya hosteli kwenye Chuo cha Afya, madarasa na maabara ya kufanyia mafunzo ya miili kwa vitendo.

Mfuko huo ambao kwa asilimia 86 umewekeza katika maeneo mbalimbali nchini, pia una mikakati mbalimbali, ikiwemo kuwekeza katika viwanda ili kutimiza azma ya Serikali ya kufikia Tanzania ya Viwanda.

Kaimu Mkurugenzi wa huduma za wanachama wa mfuko huo, Ramadhan Mkeyenge alisema alipokuwa akitembelea miradi hiyo kuwa katika mkakati huo tayari mfuko umeshafanya utafiti wa awali wa kujenga kiwanda cha chai wilayani Lushoto na kamba mkoani Tanga. Gharama za uwekezaji huo ni shilingi bilioni 7.4.

Mkeyenge alisem kuwa mfuko huo unakuwa kwa kasi na kubainisha kuwa kuanzia 2008 mpaka Oktoba 2016, umekua kwa asilimia 80; kutoka shilingi bilioni 216 mpaka kufikia trilioni 1.12 na kuufanya uwe na uwezo wa kulipa pensheni za wastaafu kwa miaka 100 ijayo bila kutetereka.

“Shughuli zetu zote tunazozifanya, zinategemea michango kutika kwa wananchama, vitega uchumi vilivyokomaa , mikopo na uwekezaji uliofanyika katika maeneo mbalimbali,

"Na kiwango kikubwa cha asilimia 44 tumewekeza kwenye amana za Serikali kutokana na kuwa ni sehemu salama zaidi na yenye kurudisha hela kwa wakati." alisema Kifungumali 

“Wanawakeza kwenye miradi mbalimbali kwa njia ya ubia upo mradi wa standi ya Msamvu Mkoani Morgoro amba ilianza mwaka 2012 na umegharimu kiasi cha shlingi bilioni 12 awamu ya kwanza, Mwanza complex-bilioni 64 na umekabidhiwa septemba mwaka huu.


Kifungumali alisema,mipango ya baadaye ya mfuko huo ni kujenga jengo la ofisi mkaoni Arusha ,kuwa na madi wa kisasa Buguruni na kuwekeza kwenye amana mbalimbali kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo