CAG ajipanga kuipekua Bodi ya Bahati Nasibu


Dotto Mwaibale

Profesa Juma Assad
KATIKA hali inayotafsiriwa kuwa watendaji wa taasisi za umma sasa wapo kwenye mazingira magumu, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeanza kuzifanyia kazi tuhuma dhidi ya Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT).

Tuhuma hizo zilizokuwa zikisambazwa kupitia mitandao ya kijamii kwa wiki mbili sasa, zinaelezwa kuwa ni majungu yasiyo rasmi na yaliyoibuliwa na watu wasiojulikana dhidi ya GBT na menejimenti yake.

Vyanzo mbalimbali vya habari kutoka ofisi ya CAG zimedokeza kwamba uchunguzi huo ulitarajiwa kuanza mapema wiki hii na utahusisha sekta kuu mbili ambazo ni ajira 
na idara ya fedha.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, CAG ameunda timu maalumu kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo zinazoikabili taasisi hiyo na menejimenti, baada ya kupokea kitu kinachoitwa waraka wenye malalamiko kadhaa.

Taarifa zinadai kuwa Mkurugenzi wa GBT Tarimba Abbas, ameidhinisha matumizi ya zaidi ya bilioni 3.8 kwa ajili ya ununuzi wa jengo la ofisi katika jingo la PSPF.

Pia watoa taarifa wamedai kwamba, amehusika na kushirikiana na bodi yake kujiongezea posho pamoja na kurekebisha mishahara yao bila kibali kutoka katika mamlaka za nchi hususan wizara ya fedha.

Tarimba mwenyewe jana alikiri kuwepo kwa taarifa hizo, lakini alikataa kuzungumzia kwa undani akidai sio msemaji na akataka atafutwe GAG.

Taarifa zaidi zimedai kwamba Tarimba, akiwa Mkurugenzi Mkuu wa GBT amewaajiri watumishi zaidi ya watano, akiwamo mtu anayetajwa kama ndugu yake wa karibu pamoja na ndugu wa baadhi ya watu waliowahi kuwa wajumbe wa bodi hiyo.

Inaelezwa pia kwamba, Tarimba alishirikiana na TRA alikwepa ulipaji wa kodi inayotokana na malipo yake ya kumalizika kwa mkataba wake wa kazi (gratuity), hatua ambayo imeikosesha serikali mapato.

Watoa taarifa walilalamikia hatua ya malipo ya milioni 4.3 kama posho ya mafuta kwa mmoja wa wakurugenzi wa bodi hiyo, hatua ambayo wamedai inaifanya taasisi hiyo 
kuwa katika mazingira magumu kiutendaji.

Hata hivyo, CAG Profesa Mussa Idrisa Assad, hakuweza kupatikana kulizungumzia suala hilo, baada ya kuelezwa kwamba yupo nje ya nchi kwa majukumu maalum ya 
kiserikali.

Uchunguzi zaidi umebaini kwamba uamuzi huo wa CAG umekuja kipindi ambacho tayari kumekuwa na waraka unaosambaa kwenye ofisi mbalimbali za Serikali na 
vyombo vya habari ikiwamo mitandao ya kijamii, unaoeleza tuhuma hizo dhidi ya menejimenti ya taasisi hiyo iliyo chini ya Wizara ya Fedha.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo