Serikali yawapanga vijana kushiriki kilimo


Emeresiana Athanas

SERIKALI imezisisitizia halmashauri zote nchini kutenga asilimia tano ya mapato yake kwa ajili ya kuwaendeleza vijana.

Pia, imesema itaweka mazingira yanayostahili katika kuwapatia vijana unafuu wanapojitoa kushiriki katika kilimo.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka wakati wa uzinduzi wa mkakati wa kuhusisha vijana katika kilimo.

Dk. Turuka alisema kuwa hadi sasa Serikali inaendelea kukamilisha mpango wa pili wa maendeleo ya kilimo wa mwaka 2016/17. Alisema mpango huo utatoa fursa kwa vijana kushiriki katika kilimo.

"Lengo la Serikali ni kuhakikisha nchi inapata maendeleo yatakayoletwa na kilimo, ambapo vijana ndio wenye nafasi kubwa katika kuchangia suala hilo," alisema.

Aliongeza kuwa taasisi za kifedha zina jukumu  la kutumia fursa ya ushiriki wa vijana katika kuwania katika kilimo na kuwataka vijana kuwa mstari wa mbele katika mageuzi kwenye sekta ya kilimo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo