Raia Cape Verde akutwa na mihadarati JNIA


Edith Msuya

RAIA wa Cape Verde, Liliana Jizas Fortes, amekamatwa na Polisi ya Viwanja vya Ndege akijaribu kupitisha dawa aina ya cocain zenye uzito wa kilo mbili na robo kupitia  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege nchini, Martin Otieno alisema jana kuwa raia huyo mwanamke alikamatwa juzi saa nane mchana akisubiri ndege ya Ethiopian Airlines ya saa 10 jioni.

"Raia huyo alitoka Brazil kwa ndege ya Shirika la Etihad na alifika Dar es Salaam na kusubiri ndege ya kwenda Malawi," alisema.

Alisema Liliana aligundulika na dawa hizo baada ya upekuzi wa kina kufanyika kwa abiria wote.  

"Tuligundua pembeni ya begi lake aliweka dawa hizo ambazo zilipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kuthibitishwa  kuwa cocain," alisema Otieno.

Alisema kukamatwa kwa Liliana ni mwendelezo wa Polisi kukagua wa mara kwa mara watu wanaopitisha vitu haramu.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo