Januari: Wanaopinga Muungano, kumsifu Nyerere wanafiki


Emeresiana Athanas

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Januari Makamba amesema watu wanaopinga Muungano huku wakimsifu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ni wanafiki.

Akizungumza Dar es Salaaam jana, Makamba alisema hata maisha aliyoishi Mwalimu Nyerere na kuyapigania wakati wa uhai wake, ni watu wachache wanaoishi maisha hayo sasa, badala yake wengine wameamua kumtumia vibaya kwa kushinikiza mambo wanayotaka au kupinga wasiyotaka.

“Huo tunaita unafiki, kwani huwezi kusema Muungano haufai, lakini Mwalimu anafaa, itakumbukwa kuwa Mwalimu alitoa machozi mwaka 1993, wakati kundi la wabunge walioitwa G55, walipoleta hoja ambazo zingesababisha kuvunjika kwa Muungano, alitoka kijijini na kuja kuhakikisha Muungano unapona na kudumu,” alisema Januari.

Alisema kutokana na hatua hiyo, Muungano ni moja ya mambo yanayotakiwa kuenziwa pamoja na maadili ya uongozi, kwani ni mambo aliyokuwa akiyasimamia.

Kwa mujibu wa Makamba, miongoni mwa mambo aliyosimamia Mwalimu Nyerere mbali na Muungano ni pamoja na kurudisha nidhamu kazini, kupinga rushwa na ufisadi ambayo kwa sasa yanasimamiwa na Rais John Magufuli.

“Yapo mambo ambayo Rais anayafanya kwa sasa kuleta nidhamu, kupinga rushwa na ufisadi ni mambo ambayo yanaturudisha kwenye misingi yake (Nyerere).

“Maadili ya umma ni niongoni mwa mambo tunayotakiwa kuyaenzi kwani ukishakuwa kiongozi wa umma, kuna baadhi ya mambo ambayo unatakiwa uyakose na bahati mbaya kwa sasa viongozi wa umma wanataka kupata vyote, heshima na utajiri,” alisema.

Alisema ipo kazi ya kuendelea kumuenzi Mwalimu, kwani kwa miaka 17 sasa tangu alivyofariki dunia bado kuna changamoto nyingi
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo