Hussein Ndubikile
January Makamba |
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,
Mazingira na Muungano, January Makamba, amesema ndani ya siku mbili, Serikali
itaeleza mkakati wa kudhibiti uzalishaji wa mifuko ya plastiki.
Mwaka jana Serikali kupitia viongozi wake
ilitoa matamko kuhusu kupiga marufuku matumizi ya mifuko hiyo, akiwamo Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliyetoa siku 90 kwa viwanda kuacha
kuzalisha kwa kuwa inachangia uchafuzi wa mazingira.
Pia, aliwataka wazalishaji kuiga mfano
wa Zanzibar ambayo imefanikiwa kudhibiti matumizi ya mifuko hiyo.
Mbali na matamko ya viongozi, Baraza la
Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) lilitoa katazo la matumizi ya
mifuko ya plastiki linalotakiwa kuanza kutumika Januari mosi ila cha kushangaza
bado inaendelea kuzalishwa na kutumika nchini.
Katazo hilo lilikuja baada ya NEMC
kubaini kuwa mifuko hiyo inasababisha uchafuzi wa mazingira kwani haiozi kwenye
udongo.
Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia
ya simu, Waziri alisema ndani ya siku hizo Serikali itaweka hadharani mipango
mikakati ya utekelezaji wa tamko la kupiga marufuku utumiaji mifuko hiyo.
Kauli hiyo imekuja baada ya tamko lake la
Aprili 19 mwaka jana bungeni ambapo alisema mwisho wa mifuko ya plastiki kutumika
itakuwa Januari mosi mwaka huu.
Akilitolea ufafanuzi suala hilo bungeni,
alisema wizara hiyo ilikuwa ikiendelea na mazungumzo kwa kushirikisha wadau na
wakati wa bajeti ya wizara yake litakuwa limekwisha ila mpaka sasa mifuko hiyo
inatumika.
0 comments:
Post a Comment