Wanane kuwania uenyekiti vyama vya siasa


Leonce Zimbandu

Sisty Nyahoza
KATIBU wa Baraza la Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, amesema wajumbe wanane wamejitokeza kugombea uenyekiti wa Baraza hilo, akiwamo aliyegombea urais kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira.

Wengine katika nafasi hiyo, ni Fahmi Davutwa ambaye ni Mwenyekiti wa UPDP, Hassan Almas (Naibu Katibu Mkuu NRA), John Cheyo (UDP), Yusuph Manyanga (Mwenyekiti SAU), John Shibuda (Katibu Mkuu Tadea), Constantine Akitanda (Mwenyekiti CCK) na Hashim Rungwe (Mwenyekiti Chauma).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari juzi, Nyahoza alisema  majina hayo yalitolewa baada ya   siku ya mwisho kwa wajumbe kuwasilisha fomu zao za kugombea.

Taarifa ilisema wajumbe wanne walijitokeza kugombea umakamu Mwenyekiti ambao ni Ameir Hassan Ameir (Katibu Mkuu Demokrasia Makini), Vuai Ali Vuai (Naibu katibu Mkuu CCM), Haji Ambari Kamis (Makamu Mwenyekiti NCCR-Mageuzi na Said Soud Said (Mwenyekiti AFP).

“Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti utafanyika Desemba 19,” alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo