Magufuli amteua Mhandisi Malaba kuongoza TCRA


RAIS John Magufuli, amemteua Mhandisi James Kilaba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi Kilaba umeanza jana. Kabla ya uteuzi huo, Kilaba alikuwa akikaimu nafasi hiyo, baada ya uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo. Dk. Ally Yahaya Simba kutenguliwa.

Simba alienguliwa katika nafasi hiyo Aprili mwaka huu, baada ya Rais kuivunja bodi ya mamlaka hiyo na kumsimamisha kazi Simba kutokana na kutosimamia ipasavyo mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS), kusababisha nchi kupoteza mapato ya takribani Sh bilioni 400 kwa mwaka.

Baada ya kuchukua uamuzi huo, alimwagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa kumteua mtu wa kukaimu nafasi hiyo na ndipo alipoteuliwa Kilaba.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo