Basi la Barcelona laua 10 ajalini


Enlesy Mbegalo

WATU 10 wamekufa huku 44 wakijeruhiwa kwenye ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Mikeja wilayani Kilwa.

Akizungumza na JAMBO LEO, kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga alisema ajali hiyo ilitokea jana saa tano asubuhi.

Alisema basi namba T 110 TWU aina ya Yutong mali ya kampuni ya Barcelona lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Newala lilipinduka na kusababisha vifo na majeruhi hao.

Kamanda Mzinga alisema chanzo cha ajali hiyo ni gurudumu la mbele kushoto kupasuka na basi hilo kupoteza mwelekeo na kupinduka.

“Ni kweli ajali hiyo imetokea leo (jana) watu 10 wamepoteza maisha papo hapo na wengine 44 kujeruhiwa na kati yao  wanawake ni 16, wanaume 10 watoto 10,” alisema Kamanda Mzinga

Pia alisema miili ya marehemu na majeruhi wako kwenye hospitali ya Kinyonga, Kilwa Kivinje.

Alisema hadi jana jioni hawakuwa wametambua majina ya marehemu wala majeruhi kutokana na madaktari kuendelea kuhudumia majeruhi.

Pia Kamanda Mzinga alisema dereva wa basi hilo naye hakuwa amefahamika bado.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo