Aliyetobolewa macho aneemeka

Salha Mohamed

MKAZI wa Dar es Salaam, Said Mrisho (34), aliyetobolewa macho na mtu anayetajwa kwa jina la  Henjewele Salum 'Scorpion'(34) amepatiwa msaada wa Sh milioni 12, Pikipiki 5, bajaj 2 pamoja na nyumba.

Mrisho alitobolewa macho Septemba 6 mwaka huu saa nne usiku na kuchomwa visu na 'Scorpion, mkazi wa Yombo Machimbo jijini humo.

Akikabidhi fedha hizo kupitia kituo cha Redio cha Clouds, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema fedha hizo Sh milioni 10 zitatumika kumuwekea macho ya bandia Mrisho, kupata elimu ya namna ya kuweza kuishi na ulemavu wa macho, huku msanii Naseeb Abdul (Diamond), akitoa Sh milioni 2.

"Nilikupa ahadi ya macho ya bandia baada ya kupata ripoti ya madaktari, Sh milioni 10 na fimbo na kupata darasa ya kujua mazingira na si kwamba tulikata tamaa kabisa lakini ripoti ya madaktari ndiyo ilitufikisha kufikiri,"alisema.

Alisema wapo wanaoandika katika mitandao ya kijamii kutaka kumsaidia Mrisho hivyo ni vema kupata taarifa ya madaktari kwani hata wao wangefurahi kuona kijana huyo akiona.

Alisema jamii inapaswa kuamini madaktari wa hapa nchini kwani wamesomea kutokana na ripoti walioitoa.

"Leo(jana) nimekuja na kutimiza ahadi yangu nimebeba Sh milioni 10 zangu ambazo nilikuahidi siku tuliyokupa majibu lakini hadi sasa machungu bado ninayo lakini sina namna nikumuachia mungu,"alisema.

Makonda alisema anatamani kuona kijana huyo anarudi katika shughuli yake ya saluni na kuwa na mradi wake na kuendeleza kile ambacho anakifanya kupitia fedha hizo.

Alifafanua kuwa, mbali na shughuli hiyo lakini amempa pikipiki alizoomba kutoka kwa wadau zitakazomsaidia, pamoja na bajaji ili kuhakikisha anaendesha maisha yake.

"Lakini niliona ni vema nikatafuta bajaj, nikapata bajaj 2 ambazo nimeziomba kwa kiongozi wa Mabohora duniani, tayari zimeshaenda kununuliwa ambazo kesho(leo) watanikabidhi, na nikitamani kutimiza ndoto yako ya kuwa na nyumba kutoka kampuni ya GSM,"alisema.

Kwa upande wake, Mrisho alisema alimshukuru Makonda kwa kutoa kiasi hicho huku akiahidi kumtaja hadi anafariki kwani amemuonesha ushirikiano katika kuhakikisha anafanikiwa kuona.

"Namshukuru sana Mkuu wangu wa mkoa,Makonda namuombea aje kuwa waziri katika nchi hii,"alisema Mrisho.

Awali Mrisho alitarajia kubadilisha makazi na kuishi nchini China huku akiwa alishaandaa ofisi ya kufanyia biashara.

"Nilikuwa tayari nabadilisha makazi niende kuishi nchini China, tayari nilishaandaa ofisi kule na tayari mtu alishatangulia na kuna mtu alishanitafutia nyumba ya mimi kuishi,"alisema.

Alisema huyo mtu aliyekuwa amemuandalia makazi na sehemu ya biashara alilia alivyosikia amepata tatizo hilo.

"Yaani nilikuwa na muda mchache sana wa kukaa hapa Tanzania yaani nilitaka kwenda kule kwani mazingira tuliyofungua ofisi yalikuwa yanalipa sana kwa kule kwasababu kule mtu mmoja anatumia gharama ndogo za maisha,"alisemana kuongeza kuwa scorpion amemuwahi kumfanyia hivyo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo