Ugomvi wa Lema, Gambo wahamia mitandaoni


Fidelis Butahe na Sharifa Marira

MENGI yametokea saa 24 baada ya kuibuka kwa mvutano kati ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kwenye uzinduzi wa mradi  wa Sh bilioni 9, ikiwemo taarifa feki ya Ikulu kuwa Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa mteule wake huyo.

Lema na mkuu huyo wa mkoa walizua tafrani hiyo juzi mjini Arusha katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa hospitali itakayohudumia bure kina mama na watoto, mbele ya wafadhili wa mradi huo, taasisi ya Martenity Africa.

Sakata hilo liibuka baada ya Gambo kutoa historia ya mradi huo, akimtaja wakili Nyanga Mawalla kuwa ndiye aliyetoa eneo kwa ajili ya ujenzi huo, jambo ambalo Lema alilipinga akisema mteule huyo wa Rais anapotosha ukweli.

Sakata hilo lilizua sintofahamu na kusababisha polisi kuingilia kati na kuwatawanya wananchi waliokuwa wakimzomea mkuu huyo wa mkoa, huku wafadhili hao wakishikwa na butwaa.

Mwendeleo wa mvutano wa viongozi hao wawili ambao wameanza uhasama siku nyingi jana ulichukua sura mpya baada ya kuiteka mitandao ya kijamii huku watu wa kada mbalimbali, wakiwemo wanasiasa, wakimshambulia Gambo na wengine kumlaumu Lema kuwa alipaswa kuwa mtulivu.

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe alisema, “Nakasirishwa sana kuona viongozi vijana wanafanya mambo ya hovyo. Mkuu wa mkoa wa Arusha mdogo wangu Mrisho Gambo una dhamana zaidi kwa vijana. Mnapofanya mambo ya kijinga mnaharibu nafasi ya vijana kuaminiwa zaidi.’’

“Kaa na Lema mnywe kahawa pale New Arusha na muanze upya. Ndugu yangu Lema nashauri punguza munkari. Juhudi zako Arusha haziwezi kufutika kirahisi. Nakushauri kaa chini na mkuu wa mkoa wako mpige mstari muanze Kazi upya kwa pamoja. Viongozi jiepusheni kuonyesha hasira zenu hadharani sio hekima’’

Mbunge wa Momba (Chadema),David Silinde aliandika katika ukurasa wake wa Facebook ‘’Hii ni edited leter (barua ya kughushi) yenye lengo la kum-prempty mhe rais asichukue hatua aliyoopanga kuichukua hii haijatengenezwa kwa lengo zuri ,kwa hili mmeharibu kila kitu’’.

Aliyekuwa Meya wa Kinondoni,Boniface Jacob,alisema hajaona jipya juu ya kilichotokea kutokana na kwamba wakuu wa mikoa na wilaya wamepewa maagizo maalum ya kukwamisha wapinzani katika maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano.

Kwa nyakati tofauti aliyekuwa Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samwel Ruhuza na Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muabhi walimpongeza Rais Magufuli kwa kutengua uteuzi wa Gambo, jambo lililoonyesha wazi kuwa walisoma taarifa feki ya Ikulu, kuiamini na kutoa maoni yao.

Akizungumzia taarifa hiyo feki ya Ikulu, mbunge wa Momba (Chadema), David Silinde katika ukurasa wake wa facebook alisema, “hii ni barua ya kughushi yenye lengo la kum-prempty Rais ili asichukue hatua aliyopanga kuichukua. Hii haijatengenezwa kwa lengo zuri. Kwa hili mmeharibu kila kitu.”

Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob alisema,“atakayekwamisha vizuri anapewa promotion, hao wakuu wa mikoa na wilaya wanapewa mafunzo maalum ya kukwamisha wapinzani katika maendeleo ,atakayeonekana anawapa ushirikiano atahamishwa eneo hilo ili aletwe mvurugaji’’

Jacob ambaye ni diwani wa Kata ya Ubungo, alisema Serikali haijali juu ya kukosa au kupoteza mradi wa mabilioni ya fedha  kutoka kwa wahisani hao na kudai aliwahi kushuhudia wafadhili wakielezwa kuondoa Sh bilioni 3.2 katika manispaa aliyokuwa anaiongoza.
Mwisho.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo